In Summary

Jaji Weldon Korir alisimamisha mashtaka dhidi yake hadi mizozo yote ya kiraia, ya kibiashara na ya kifamilia inayogonganisha Linturi dhidi ya Maryan Kettany isikizwe na kuamuliwa.

Seneta wa Meru Mithika Linturi

Mahakama kuu imetoa agizo la kuwazuia mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP na DCI kumkamata na kumshtaki Seneta wa Meru Mithika Linturi kuhusu madai ya ulaghai wa shilingi milioni 530.

Jaji Weldon Korir alisimamisha mashtaka dhidi yake hadi mizozo yote ya kiraia, ya kibiashara na ya kifamilia inayogonganisha Linturi dhidi ya Maryan Kettany isikizwe na kuamuliwa.

Rasimu ya stakabadhi ya mashtaka inaonyesha Linturi alipaswa kukabiliwa na mashtaka angalau 38 kwa madi ya kutoa habari za uwongo kwa mtu aliyeajiriwa katika utumishi wa umma, kupata mkopo kwa njia ya udanganyifu, matumizi mabaya ya ofisi, kughushi kati miongoni mwa madai mengine mengi.
View Comments