In Summary

• Licha ya kuwa walikuwa wafungwa ,waliendelea kupata watoto na wake zao ambao wapo katika eneo la Wapalestina la Gaza na West Bank sehemu zinazokaliwa na waisraeli.

• Huduma ya Magereza Israeli (IPS) ilitia shaka uwezekano wa mtu kupitisha manii kwa njia ya magendo.

Mamake Dallal, anasema kumzaa mtoto wake huyo ni 'zawadi' kutoka kwa Mungu

Mwanzoni ungemuambia mtu kwamba jambo hili lilikuwa likitendeka basi ungekumbana na pingamizi si haba kuhusu uwezekano na hata ukweli wa kile ambaco wafungwa walikuwa wakifanya waiwa ndani ya mageeza ya Israel.

Licha ya kuwa walikuwa wafungwa ,waliendelea kupata watoto na wake zao ambao wapo katika eneo la Wapalestina la Gaza na West Bank sehemu zinazokaliwa na waisraeli.

Ripoti za mwanzo mwaka wa 2013 kwamba wafungwa walikuwa wakiweza kutoa mbegu za kiume na kuzificha kwenye kila aina ya chupa na kisha kuzitoa magerezani kisiri hadi kwa wake zao ili wapandikizwe mimba kupitia IVF zilipokelewa kwa njia ya kupuuzwa.

Maafisa wa Israel wenyewe walisema kwamba haingezekana kwamba mfungwa angeachiliwa huru kisha aondoke akiwa na chupa zenye manii kuwapelekea wake za wafungwa wenzake waliobaki jela.

Inavyofanyika

Muhannad Ziben sasa ana umri wa miaka tisa . Alizaliwa katika hospitali Nablus's al-Arabia agosti mwaka wa 2012.

Mamake Dallal anasema kumzaa mtoto wake huyo ni 'zawadi' kutoka kwa Mungu kwani babake yupo jela.Anahudumia vifungo 32 vya maisha katika gereza na Israel baada ya kushtumiwa kwa kuhusika na shambulizi la kigaidi dhidi ya Israel mwaka wa 1997 huko Jerusalem .Lakini aliwezaje kupata mimba na kumzaa Ziben?

Dallal anasema aliweza kupata mimba baada ya manii ya mumewe kuletwa kimagendo kutoka gereza la Israel na kisha akatumia mbinu ya upandikizaji au IVF kuibeba mimba ile na kumzaa mtoto wake .

Sio yeye pekee anayefanya hivyo kwani mamia ya wanaume wa Kipalestina anaohudumua vifungo katika jela za Israel wameendelea kuwazaa watoto na wake zao wakiwa jela kwa kutumia mbinu hiyo .

Manii inavukishwa kutoka jela na kupewa mtu ambaye ameshahudumia kifungo chake anayetoka jela .Wakati mwingine jamaa wanaoruhusiwa kuwatembelea wafungwa ndio hukabidhiwa 'mali' hiyo muhimu ili kuhakikisha kwamba Waalestina wanaendeleeza vizazi vyao hata chini ya utawala wa Israel na hali ngumu ya maisha katika sehemu zao .

Alipozungumza na BBC mwaka wa 2013 Dallal alisema ;

"Muhannad ni zawadi kutoka kwa Mungu, Laini furaha yangu haijakamilika bila mume wake kuwa hapa na mimi'

Kisa hicho cha Dallal kiliangaziwa sana na vyombo vya habari.

Tangu wakati huo, BBC ilizungumza na madaktari wawili wa uzazi katika Ukingo wa Magharibi ambao wanasema sasa kuna mamia ya wanawake Kipalestina ambao wamepata ujauzito wakitumia manii iliyosafirishwa nje ya jela za Israeli.

"Kwa kweli, sijui wanafanyaje na sitaki kujua jinsi wanavyofanya," alisema Dk Salem Abu Khaizaran, mmoja wa madaktari wa uzazi ambaye amekuwa akiwasaidia wanawake.

"Sitaki kuingia kwenye siasa. Ninafanya hivyo kwa sababu za kibinadamu tu, kusaidia tu wanawake hawa. Kila mtu anawashughulikia sana wafungwa, lakini wanawake hawa wanateseka sana."

'Inawezekana kweli?'

Huduma ya Magereza Israeli (IPS) ilitia shaka uwezekano wa mtu kupitisha manii kwa njia ya magendo.

"Mtu hawezi kusema haikutokea. Walakini, ni vigumu kuamini inaweza kutokea kwa sababu ya hatua kali za usalama zinazochukuliwa wakati wa mikutano ya wafungwa na jamaa zao na kwa ujumla," msemaji wa Mamlaka ya magereza wakati huo alisema

Alisema kuwa hakuna utangamano wa ana kwa ana ati ya wafungwa na familia zao, isipokuwa kwa dakika 10 za mwisho za ziara hiyo, wakati ambao watoto wa mfungwa, ikiwa ni chini ya umri wa miaka nane, wanaruhusiwa kupatana na baba yao.

Tofauti na wafungwa wengine wa Israeli, Wapalestina ambao wamefungwa kwa kile Israeli inaita makosa ya usalama hawaruhusiwi ziara za ndoa ambapo wanaweza kushiriki tendo la ndoa na wake zao .

IPS haikuweza kusema ikiwa Wapalestina wowote waliofungwa kwa makosa ya jinai wamewahi kupewa ziara kama hizo.

"Wafungwa wa Israeli wanapata haki nyingi. Wanaruhusiwa kutoka gerezani kwa ziara za nyumbani. Wana uwezo wa kuwa na wake zao," alisema Waziri wa wakati huo wa Magereza wa Mamlaka ya Palestina Issa Qaraqa.

Anaongeza kuwa Yigal Amir, mwenye msimamo mkali wa kidini na raia wa Israeli ambaye alifungwa kifungo cha maisha kwa kumuua Waziri Mkuu wa Israeli Yitzhak Rabin mnamo 1995, aliruhusiwa kuoa na kuwa na ziara za kindoa zilizosababisha kuzaliwa kwa mtoto wa kiume mnamo 2007.

Dk Abu Khaizaran anaamini Wapalestina wanapaswa kupewa haki hiyo. Anasema hadi hapo itakapotokea, wafungwa wa Palestina wataendelea kujaribu kusafirisha manii nje ya jela kwa wake zao.

Ni kazi ngumu kweli

Daktari anasema wanawake huleta manii kwenye kliniki yake kwa chochote kutoka chupa ndogo hadi vikombe vya plastiki.

Dk Abu Khaizaran anasema, katika hali nzuri, manii inaweza kuishi hadi masaa 48 kabla ya kugandishwa ili kufanya matibabu ya IVF.

Kawaida anasema wanawake wanaweza kuipeleka kwa wakati mfupi kuliko huo lakini wakati mwingine mbegu za kiume hazifiki katika hali nzuri ya kutosha na wanawake wanaambiwa lazima wajaribu tena.

Kliniki hiyo inasita kutoa matibabu kwa wanawake ambao tayari wana watoto wengi au ambao waume zao wanatumikia vifungo vifupi tu.

Kabla ya IVF kuendelea mbele daktari anauliza kuona watu wawili wa familia za mume na mke ambao wanaweza kushuhudia kwamba manii ni ya kweli.

Image: GETTY IMAGES

Wanawake pia wanashauriwa kueneza habari juu ya kile wanajiandaa kufanya.

"Wakati kijiji kizima kinajua mume wa mwanamke amekuwa gerezani kwa miaka 10 au 15 hatutaki atembee barabarani akiwa mjamzito," anasema Dk Abu Khaizaran.

"Tunamshauri mwanamke kurudi kijijini kwake na kumwambia kila mtu kuwa ana sampuli kutoka kwa mumewe na kwamba ana mpango wa kufanya IVF katika miezi michache."

Anasema kwa njia hii inaepuka uvumi ikidokeza mwanamke anaweza kuwa alikuwa akimdanganya mumewe wakati mume wake yupo gerezani

View Comments