In Summary

•Vyama vya PEP na UDA ambazo zinahusishwa na naibu rais vimeteua wagombea viti wawili tofauti kwenye uchaguzi mdogo wa Kiambaa

•Kwenye uchaguzi mdogo wa Juja, chama cha UDA kilikuwa kinamuunga mkono George Koimburi kwani hakikuwa kimezindua mgombeaji

dp ruto
Image: Hisani, The Star

Mzozano umeibuka kwenye kambi ya naibu rais almaarufu kama 'Tangatanga' baada ya vyama mbili zinazojihusisha naye kuteua wagombea viti  tofauti katika eneo bunge la Kiambaa.

Baada ya kupata ushindi mkubwa katika eneo bunge la Juja, chama cha People’s Empowerment Party (PEP)  kimeonekana kupata motisha huku kikizindua mgombeaji kwenye uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Kiambaa.

PEP inayoongozwa na mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria imetangaza kuwa Raymond Kuria Mwaura ndiye atakayepeperusha bendera katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe 15 Julai.

Chama hicho kimeonekana kupata misuli baada ya George Koimburi kuibuka mshindi kwa asilimia 56% kwenye uchaguzi uliofanyika Juja siku ya Jumanne.

- Mgombeaji Raymond Kuria wa PEP
- John Njuguna wa UDA

Kwenye uchaguzi mdogo wa Juja, chama cha UDA kilikuwa kinamuunga mkono George Koimburi kwani hakikuwa kimezindua mgombeaji.

Raymond atakuwa akikabilia na mgombeaji kwa tikiti ya UDA, John Njuguna na mgombeaji kwa tikiti ya Jubilee na ambaye bado hajajulikana huku ikitangazwa kuwa mpeperushaji bendera wake atatambulikana kupitia njia ya mahojiano.

Kuria amekashifiwa na baadhi ya wafuasi wa chama cha UDA ikiwemo Rigathi Gachagua huku ikisemekana kuwa anatia doa ushirikiano ulioko katika ya vyama hivyo viwili.

Gachagua amesisitiza kuwa mgombeaji aliyeteuliwa na muungano wa ‘Hustlers’ ni John Njuguna na kutupilia mbali ugombeaji wa Raymond Kuria.

View Comments