In Summary
  • Kenya imerekodi visa 111 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 1,948 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 168,543 kutoka kwa sampuli 1,783,374
  • Wagonjwa 121 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
  • Idadi ya waliopokea chanjo ya covid-19 imefika 954,515
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya imerekodi visa 111 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 1,948 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 168,543 kutoka kwa sampuli 1,783,374.

Katika visa hivi vipya, 108 ni raia wa Kenya huku 3 wakiwa raia wa kigeni, 62 ni wa kiume na 49 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miaka 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 89.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 142 wamepona virusi vya corona,137 walipona wakiwa nyumbani huku 5 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 114,679 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 14 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,073 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,086 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,770 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 121 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya waliopokea chanjo ya covid-19 imefika 954,515.

View Comments