In Summary
  • Mgonjwa mwenye umri wa miezi 4 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 98
  • Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 10.3%

Kenya imerekodi visa 382 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 3,719 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 168,925 kutoka kwa sampuli 1,787,093.

Katika visa hivi vipya, 366 ni raia wa Kenya huku 16 wakiwa raia wa kigeni, 226 ni wa kiume na 156 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa miezi 4 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 98.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 10.3%.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 1,134 wamepona virusi vya corona,875 walipona wakiwa nyumbani huku 259 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 115,813 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 14 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,087 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,079 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,756 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 113 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

 

View Comments