In Summary
  • Kenya imerekodi visa 88 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 1,668 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 170,735 kutoka kwa sampuli 1,811,558
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya imerekodi visa 88 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 1,668 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 170,735 kutoka kwa sampuli 1,811,558.

Katika visa hivi vipya, 87 ni raia wa Kenya huku 1 akiwa raia wa kigeni, 56 ni wa kiume na 32 ni wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa miaka 6 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 84.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 5.3%.

Kulingana na takwimu za wizara ya afya watu 71 wamepona virusi vya corona,64  walipona wakiwa nyumbani huku 7  wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 116,847 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 15 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,172 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,237 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,661 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 93 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU

 

 

View Comments