In Summary
  • Watu 349 wapatikana na virusi vya corona, hii ni kutoka kwa sampuli 4,208 zilizopimwa chini ya saa 24
  • Idadi JUmla ya watu walioambukizwa virusi vya corona imefika 171,084, huku idadi ya sampuli zilizopimwa ikifika 1,815,766
  • Mgonjwa mwenye umri wa siku saba huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 90

Watu 349 wapatikana na virusi vya corona, hii ni kutoka kwa sampuli 4,208 zilizopimwa chini ya saa 24.

Idadi JUmla ya watu walioambukizwa virusi vya corona imefika 171,084, huku idadi ya sampuli zilizopimwa ikifika 1,815,766.

Kati ya maambukizi hayo ya jumanne  327 ni raia wa kenya ilhai 22 ni raia wa kigeni, wagonjwa 196 ni wakiume ilhali 153ni wa kike.

Mgonjwa mwenye umri wa siku saba huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 90.

Kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa 80, huku asilimia ya maambukizi ikifika 8.3%.

Kulingana na wizara ya afya watu 176 wamepona maradhi ya corona, 144 wamepona huku wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 32 wakiruhusiwa kuenda nyumbani.

Idadi jumla ya watu waliopona imefika 117,023.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 16 wameaga dunia kutokana na corona, idadi ya walioaga dunia kwa sasa imefika 3,188.

Wagonjwa 1,257 wamelazwa hospitalini huku 4,704 wakijitenga nyumbani, kuna wagonjwa 92 katika kitengo cha wagonjwa mahututi.

 

 

 

View Comments