In Summary

•Okimaru ambaye ni afisa katika kituo cha polisi cha Dabel kilicho pande za Moyale alikamatwa usiku wa Mei 14 na maafisa wa DCI kwa kutuhumiwa kumuua Mungai.

•.Inadaiwa kuwa mshukiwa pamoja na wengine ambao hawakufikishwa kotini walimuua Joshua Mwangi usiku wa Aprili 18/19 2021 katika eneo la Olekasasi pande za Ongata Rongai.

Konstabo Edwin Okimaru mbele ya mahakama kuu ya Machakos
Image: Hisani

Afisa wa polisi aliyekamatwa kwa tuhuma za kumuua kondakta wa Stage One pande za Ongata Rongai amekanusha mashtaka hayo katika mahakama kuu ya Machakos.

Konstebo Edwin Okimaru alifikishwa mahakamani siku ya Jumatano na kusomewa shtaka la kumuua Joshua Mungai ambalo alikanusha.

Okimaru ambaye ni afisa katika kituo cha polisi cha Dabel kilicho pande za Moyale alikamatwa usiku wa Mei 14 na maafisa wa DCI kwa kutuhumiwa kumuua Mungai ambaye alikuwa manamba katika kituo cha magari cha stage 1 mtaa wa Ongata Rongai.

Mshukiwa alifikshwa mbele ya jaji George Odunga.

Upelelezi uliofanywa na maafisa wa DCI, idara ya kupeleleza uhalifu wa kimitandao na ofisi ya ujasusi ulionyesha kuwa mshukiwa alikuwa katika eneo la mauaji hayo

.Inadaiwa kuwa mshukiwa pamoja na wengine ambao hawakufikishwa kotini walimuua Joshua Mwangi usiku wa Aprili 18/19 2021 katika eneo la Olekasasi pande za Ongata Rongai.

Soma zaidi  hapa kuhusu mauaji hayo...

Hata hivyo, kupitia mawakali wake Lydia Abuya na Emmanuel Mwangi mshukiwa alikanusha mashtaka hayo.

Jaji Odunga alielekeza kesi hiyo kutajwa tarehe 7 Julai ili kuamua hali ya dhamana kama walivyoagiza mawakili wa mshukiwa.

View Comments