In Summary
  • Kenya siku ya JUmatatu imerekodi visa 218 vipya vya maambukizi ya corona, kutoka kwa sampuli 2,577 zilizopimwa ndani ya saa 24 zilizopita
  • Idadi jumla ya maambukizi ya corona imefika 179,293 huku jumla idadi ya sampuli ikifika 1,907,096
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya siku ya JUmatatu imerekodi visa 218 vipya vya maambukizi ya corona, kutoka kwa sampuli 2,577 zilizopimwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya maambukizi ya corona imefika 179,293 huku jumla idadi ya sampuli ikifika 1,907,096. 

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 206 ni wakenya ilhali 12 ni raia wa kigeni, vivle vile 117 ni wanaume ilhali 101 ni wa kike.

Pia mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 7 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 85.

Kulingana na wizara ya afya, maambukizi hayo ni kutoka kwa kaunti  Nairobi 119, Siaya 26, Kisii 20, Uasin Gishu 15, Homa Bay 10, Nakuru 6, Kajiado 4, Kakamega 4, Makueni 2, Nyandarua 2, Migori 1, Mombasa 1, Nandi 1, Vihiga 1, Bomet 1, Kericho 1, Kiambu 1, Kisumu 1, Laikipia 1 na Machakos.

Watu 261 wamepona corona na kufikisha idadi jumla ya 122,965 ya watu waliopona maradhi ya corona.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 5 wamepoteza maisha yao kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 3,461 ya watu walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 1,074 ambao wamelazwa hospitali huku 5,638 wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani.

Wagonjwa  103 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi,

 

 

View Comments