In Summary

• Programu hii mpya itawapa wateja suluhisho rahisi, ni ya kufurahisha, salama na rahisi kutumia.

• Programu mpya ya M-Pesa inampa mteja uwezo wa kufanikisha mengi zaidi katika maongezi yake, nyumbani au kutoka mahali popote alipo kwa urahisi.

Afisa mkuu mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa akizindua programu ya M-Pesa mnamo Juni 23, 2021. Picha: Twitter / Safaricom

Kampuni ya mawasiliano Safaricom siku ya Jumatano ilizindua App mpya ya M-Pesa, ili kuongeza uzoefu wa wateja kila wakati wanapotumia huduma hiyo.

Programu hii mpya itawapa wateja suluhisho rahisi, ni ya kufurahisha, salama na rahisi kutumia.

Wakati wa uzinduzi wa programu hii kwa njia ya video, Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa alisema kampuni hiyo inaanzisha matumizi ya programu, ambayo inamaanisha wafanyabiashara watakuwa na programu ya kipekee ambapo wanaweza kusasisha leseni, kusimamia na kulipa bili zao, kushirikiana na wateja miongoni mwa shughuli nyingine nyingi.

"Programu ya kibiashara ya M-Pesa itawawezesha na kuwapa wafanyibiashara zana madhubuti za kusimamia na kukuza biashara zao. Hatimaye, lengo letu ni kwamba kwa kila Shilingi moja biashara inakusanya kwa M-Pesa, wanapaswa kupata Shilingi 5 za ziada," Ndegwa alisema.

Kampuni ya Safaricom ilisema itaangazia sana programu, kuunda mfumo thabiti wa Dijiti kwa wateja wao.

Ndegwa alisema kuwa mbali na kukusanya malipo, wafanyabiashara wanaweza kulipia vifaa, kulipa mshahara, kununua kutoka kwa biashara zingine na wanaweza kutumia pesa anayolipa mteja mara moja; sio lazima wasubiri siku au saa baada ya malipo kufanywa.

"Tunafurahi kuhusu ubunifu huu ambao utatusaidia kuwa shirika linalowajali wateja, la kwanza-la dijitali ili tuweze kuunda kampuni ya teknolojia inayoongozwa na kusudi fulani."

“Kwa miezi michache iliyopita, tumekuwa tukijaribu programu mpya ya M-Pesa na zaidi ya wateja milioni 1 ambao wamekuwa wakitumia huduma hii. Napenda kuwashukuru kwa dhati kwa sababu wametupa maoni juu ya nini cha kuboresha,”

Mkurugenzi Mtendaji wa M-Pesa kanda ya Africa, Sitoyo Lopokoiyit, alisema.

Aliongeza kuwa programu ya M-Pesa inampa mteja uwezo wa kufanikisha mengi zaidi katika maongezi yake, nyumbani au kutoka mahali popote alipo kwa urahisi.

"Tumeunda programu ya M-Pesa kutoa muundo wa kisasa, wa kufurahisha na angavu ambao unaboresha urahisi na usalama. Ubunifu mpya huondoa makosa na kutuwezesha kuongeza huduma mpya. Sitoyo alisema.

View Comments