In Summary

• WHO imezitaka nchi za Afrika kuzingatia hatua za usalama huku zikijiandaa kwa mpango mpya wa utoaji wa chanjo kwa ajili ya kukabiliana na virusi.

Shirika la afya duniani limetahadharisha kuwa hali mbaya zaidi ya ugonjwa wa corona itashuhudiwa barani, huku mataifa memgi ya bara hilo yakikabiliana na aina ya corona inayofahamika kama Covid-19 Delta inayoendelea kusambaa.

WHO imezitaka nchi za Afrika kuzingatia hatua za usalama huku zikijiandaa kwa mpango mpya wa utoaji wa chanjo kwa ajili ya kukabiliana na virusi.

WHO inasema kuwa wiki ya mwisho ya mwezi Juni ilikuwa ni wiki mbaya zaidi kwa maambukizi katika bara la Afrika.

Mkurugenzi wa kanda ya Afrika Dkt Matsidisho Moeti amesema kuwa maambukizi mapya ya corona yanaongezeka mara dufu kila baada ya siku 18. Ongezeko kubwa la wimbi la tatu la maambukizi linaweza kutokea wiki chache zijazo.

Katika baadhi ya nchi, kama vile Namibia na Tunisia, hospitali zinahangaika kukabiliana na idadi kubwa ya wagonjwa.

Huku chini ya 2% ya watu wakiwa ndio waliopata chanjo kamili, wengi wataendelea kukabiliwa na hatari ya kuugua sana corona.

Lakini WHO ina matumaini kwamba misaada kutoka Marekani nan chi nyinginge kupitia mpango wa usambazaji wachanjoCovax usaidia nchi kuinua kampeni za chanjo.

View Comments