In Summary
  • Kenya imesajili visa vipya 591 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,737 chini ya saa 24 zilizopita
  • Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 204,271 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 12.5%
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Kenya imesajili visa vipya 591 vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,737 chini ya saa 24 zilizopita.

Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 204,271 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 12.5%.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 575 ni wakenya ilhali 16 ni raia wa kigeni,316 ni wanaume huku 275 wakiwa wanawake.

Kulingana na wizara ya afya watu 24 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 3,970 ya walioaga dunia.

Jumla ya wagonjwa 561 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 189,692, 469 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 92 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,483 ambao wamelazwa hospitalini,4,021 wamejitenga nyumbani.

Pia kuna wagonjwa 189 kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 1,726,937

 

 

 

 

 

View Comments