In Summary

•Kufikia sasa Kenya imepokea msaada wa dozi 817,000 kutoka kwa serikali ya Uingereza kwani dozi zingine 410,000 zilikuwa zimewasili nchini mwishoni mwa mwezi Julai.

Daktari Patrick Amoth akihutubia wanahabari baada ya kupokea chanjo zilizowasili
Image: TWITTER//MOH

Kenya imepokea msaada zaidi wa dozi 407, 000 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Uingereza.

Shehena hiyo  iliwasili katika uwanja wa ndege wa JIKA alfajiri ya Jumatano na kupokewa na mkurugenzi mkuu wa afya nchini Daktari Patrick Amoth.

Kufikia sasa Kenya imepokea msaada wa dozi 817,000 kutoka kwa serikali ya Uingereza kwani dozi zingine 410,000 zilikuwa zimewasili nchini mwishoni mwa mwezi Julai. Jumla ya dozi 2,730,100 zimeweza kufika nchini kutoka mataifa mbalimbali kufikia sasa.

Daktari Amoth alishukuru serikali ya Uingereza , shirika la afya duniani, UNICEF na washirika wengine ambao wamefanikisha kufika kwa dozi hizo.

TWITTER//MOH - Daktari Patrick Amoth akihutubia wanahabari baada ya kupokea chanjo zilizowasili

Amoth amesema kuwa Kenya inatarajia kupokea dozi milioni 1.7 za chanjo aina ya Moderna, dozi 393,000 za Johnson & Johnson na dozi milioni 1.8 za Pfizer hivi karibuni.

Chanjo hizo zinatazamiwa kuboresha juhudi za serikali ya Kenya katika kupigana na ongezeko la maambukizi ya Corona.

Kufikia sasa takriban watu 2,101,403 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona nchini.

View Comments