In Summary

Katika hati yake ya kiapo kujibu mashtaka, Kasisi huyo alisema kwamba alikuwa na uhusiano wa muda mfupi na mwanamke huyo uliomalizika mwaka 2018.

Bishop David Muriithi wa kanisa la House of Grace

Askofu wa kanisa la House of Grace David Muriithi amethibitisha kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wa kiume ambaye alipata nje ya ndoa na mwanamke ambaye alimshtaki mapema mwezi huu.

Muriithi alisema atachukua jukumu la mtoto wake na mwanamke huyo lakini atamlipa tu Shilingi 10,000 kila mwezi kwa sababu yeye ni masikini na anategemea watu wenye nia njema kuishi.

"Ninajitolea kuchukua jukumu kamili la kugharamia maisha ya mtoto mchanga na vile vile kulipa 10,000 kwa mwezi kwa utunzaji wa mtoto kulingana na uwezo wangu mdogo na jukumu la familia," alisema.

Katika hati yake ya kiapo kujibu mashtaka, Kasisi huyo alisema kwamba alikuwa na uhusiano wa muda mfupi na mwanamke huyo uliomalizika mwaka 2018.

"Wakati nilikutana na mwanamke huyu alikuwa akiishi katika nyumba yake ya kukodisha na mtoto wake mwingine wa kiume aliyepata katika uhusiano tofauti na alijilipia kodi yake mwenyewe," hati yake ya kiapo inasoma.

Muriithi hata hivyo anasema kuwa hakujua kwamba mwanamke huyo alikuwa mjamzito na hakuwahi kumfunulia kuwa alikuwa na mimba.

Muriithi amemshtumu mwanamke huyo kwa kumtumia mtoto wao kumpora pesa kwani anafikiria yeye ni tajiri.

View Comments