In Summary

• Ruto alisema  BBI ilikuwa "ulaghai mkubwa na hatari zaidi"

Naibu rais William Ruto
Image: DP Ruto/twitter

Wafuasi wa mchakato wa uiano BBI, wanafaa kuacha kusema uwongo kwamba hiyo ndio njia ya pekee ya kuongeza mgao katika serikali za kaunti.

Akizungumza katika makazi yake rasmi mtaani Karen Naibu rais William Ruto alisema watetezi wa BBI wana fursa ya kuwasilisha mapendekezo ya kuongeza mgao wa kaunti kwa ikiwa walikuwa wakweli kufanikisha azimio hilo.

"Kaunti bado zinaweza kupewa fedha zaidi kupitia Bunge bila kufanyika kwa kura ya maamuzi chini ya BBI," alisema.

Alielezea kuwa hata kuundwa kwa maeneo bunge ya ziada kunawezekana bila kuipitisha nchi katika gharama za kuandaa kura ya maamzi ili kurekebisha Katiba.

"Ikiwa Wakenya walikuwa wanahitaji maeneo bunge zaidi, basi Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ingeshirikishwa."

Rais Uhuru Kenyatta atia saini wakati wa hafla ya kuzindua saini za kufanikisha ripoti ya BBI. (Picha PSU)

Ruto alisema kuwa wananchi wanafaa kujiupusha na udanganyifu wa hovyo kutoka kwa viongozi wengine ili kupata ushabiki wa kisiasa baada ya kushindwa kuuza BBI kwa Wakenya.

Alisema watetezi wa BBI wanapaswa kuomba msamaha kwa Wakenya kwa kuhujumu ajenda Kubwa Nne za serikali.

"Ingeweza kuunda mamilioni ya fursa za kazi badala ya kuhakikisha kwamba Wakenya wote wanapata huduma ya matibabu ya bei nafuu. Lakini mafanikio haya yote yalipungua kwa sababu ya BBI, ”akaongeza.

Hata kwa vitisho na rasilimali kubwa iliyotumiwa, Naibu Rais alisema kuwa "hakuna njia BBI itapita."

Alisema BBI ilikuwa "ulaghai mkubwa na jukumu hatari zaidi" kuwahi kutekelezwa Kenya ambayo ingeharibu maoni yake ya kidemokrasi kwa sababu ya kuanzishwa kwa rais wa kifalme.

"Kwa hivyo lazima ikose, na kufa milele."

View Comments