In Summary

• Bunduki tatu za AK-47, bunduki moja ya Mark4, risasi 203, magazini tisa za AK-47 zilipatikana katika uvamizi wa saa kumi na moja asubuhi.

•Wiki mbili zilizopita, serikali ilizindua mwezi wa msamaha kwa watu wenye silaha haramu.

Silaha hatari zilizomaswa
Image: DCI

Watu wawili wamekamatwa na kasha la silaha kupatikana eneo la Garbatulla, kaunti ya Isiolo.

Abdi Guyo 35, na Amina Mohamed 30, walikamatwa katika oparesheni kali asubuhi na mapema.

Mkurugenzi wa DCI George Kinoti alisema maafisa walidokezewa kuhusu kuwepo kwa silaha hizo na wananchi.

"Kunaswa kwa silaha hizo hatari kulijiri baada ya maafisa wa polisi waliokuwa wamepewa vidokezo na wananchi, kuvamia nyumba moja viungani mwa mji wa Kinna, wakati wa alfajiri," Kinoti alisema.

Bunduki tatu za AK-47, bunduki moja ya Mark4, risasi 203, magazini tisa za AK-47 zilipatikana katika uvamizi wa saa kumi na moja asubuhi.

Image: DCI

Pia walipata misokoto sita ya bangi na pikipiki mbili zisizo na nambari za usajili ambazo huenda zilikuwa za kutumiwa wakati wa kutoroka pia zilinaswa katika oparesheni hiyo.

"Wapelelezi katika eneo la Garbatulla kwa sasa wanawahoji washukiwa," Kinoti alisema.

Wiki mbili zilizopita, serikali ilizindua mwezi wa msamaha kwa watu wenye silaha haramu.

Waziri wa usalama Fred Matiang’i alizindua mpango huo na kutaka umma kutumia fursa ya msamaha, kushirikiana na maafisa wa usalama na kurudisha silaha haramu.

Wale ambao wanarudisha bunduki kabla ya Septemba 30 wamehakikishiwa msamaha.

View Comments