In Summary

•Inaripotiwa kwamba afisa huyo alishiriki kwenye mabishano makali na mpenzi wake mwendo wa usiku wa manane kabla ya  ghadhabu kumshinikiza kutoa kisu na kumdunga hadi kifo.

•Oyugi alifichua kwamba afisa marehemu alikuwa na matatizo kwenye ndoa yake kwani mkewe na mtoto mmoja walikuwa wametoroka nyumbani baada ya kugundua kuwa alikuwa na mipango wa kando.

crime scene 1

Afisa mmoja wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Masalani kaunti ya Garissa anaripotiwa kijitoa uhai kwa njia ya kujilipua kwa bomu la mkono punde baada ya kuua mpenzi wake.

Inaripotiwa kwamba afisa huyo alishiriki kwenye mabishano makali na mpenzi wake mwendo wa usiku wa manane kabla ya  ghadhabu kumshinikiza kutoa kisu na kumdunga hadi kifo.

Punde baada ya kutekeleza mauaji hayo afisa huyo anadaiwa kutumia bomu la mkono kujilipua na akafariki papo hapo.

Mshtuko mkubwa wa bomu ambalo marehemu anadaiwa kutumia kujitoa uhai ulisababisha hofu kubwa kwa wakazi wa eneo hilo la Masalani ambao walidhani walikuwa wameshambuliwa na Al Shabaab.

Maafisa wenza wa marehemu ni miongoni mwa waliokimbia mafichoni baada ya kushtuliwa na mlio huo ila walipojipanga  kubaini kilichokuwa kinaendelea wakagundua kwamba ni mwenzao alikuwa amelipua bomu.

Alipokuwa anathibitisha tukio hilo, kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Ijara William Oyugi alisema kwamba polisi walipofika kwenye eneo la tukio walipata miili ya wapenzi hao wawili ikiwa imezungukwa na dimbwi la damu.

Mwili wa afisa yule ulikuwa umejawa na majeraha ya moto ilhali ule wa mpenzi wake ulikuwa na majeraha ya kudungwa kwa kisu.

Oyugi alisema kwamba huenda afisa yule aliamua kujitoa uhai kutokana na majuto alipogundua kuwa mpenzi wake alikuwa amekata roho kufuatia kitendo cha unyama alichokuwa ametekeleza.

Alifichua kwamba afisa marehemu alikuwa na matatizo kwenye ndoa yake kwani mkewe na mtoto mmoja walikuwa wametoroka nyumbani baada ya kugundua kuwa alikuwa na mipango wa kando.

Miili ya marehemu ilipelekwa katika mochari moja maeneo ya Mwingi huku uchunguzi wa maiti ukisubiri kufanywa.

View Comments