In Summary

•Kufikia sasa watu 3, 504, 400 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 1, 425, 936 wakiwa wamepokea dozi zote mbili

Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya Corona kwa sasa ni 1% huku wizara ya afya ikitangaza visa vipya  44 nchini kutoka kwa sampuli ya watu 4,238 ambao wameweza kupimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 ambacho kimepita.

Kufikia sasa Kenya imewahi kurekodi visa 252, 672 kutoka kwa jumla ya vipimo 2, 673, 705 ambavyo vimewahi kufanywa tangu mwanzo wa janga la Corona.

Kaunti ya Nyamira imeripoti visa vingi zaidi (11) ikifuatwa na Nairobi na Isiolo ambazo zimeandikisha visa 9 na 6 mtawalia.

Wagonjwa 247 wameweza kupona, 200 wakiponea nyumbani huku 47 wakipona kutoka vituo mbalimbali vya afya nchini. Kufikia sasa watu 246, 274 wamewahi kupona maradhi hayo.

Idadi ya vifo nchini kutokana na COVID 19 imefikia 5, 257 baada ya vifo 2 zaidi kuripotiwa leo.

Kwa sasa wagonjwa 496 wanahudumiwa hospitalini huku wengine 1365 wakipokea matibabu kutoka manyumbani kwao. Wagonjwa 27 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Kufikia sasa watu 3, 504, 400 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 1, 425, 936 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

View Comments