logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Polisi wanaohusishwa na mauaji ya ndugu wawili kutoka Kianjokoma waachiliwa kwa dhamana

Jaji Daniel Ogembo hata hivyo amewazuia sita hao dhidi ya kuenda katika eneo la Kianjokoma ambapo mauaji hayo yalitokea.

image
na SAMUEL MAINA

Habari04 November 2021 - 13:23

Muhtasari


  • • Jaji Daniel Ogembo hata hivyo amewazuia sita hao dhidi ya kuenda katika eneo la Kianjokoma ambapo mauaji hayo yalitokea.
Polisi sita ambao walishtakiwa kwa mauaji ya ndugu wawili Embu wakiwa mahakamani

Habari na Annette Wambulwa

Maafisa sita wanaohusishwa na mauaji ya ndugu wawili katika eneo la Kianjokoma, kaunti ya Embu wameachiliwa kwa dhamana.

Sita hao; Benson Mputhia, Consolata Kariuki, Nicholas Cheruiyot, Martin Wanyama, Lilian Chemuna na James Mwaniki wameagizwa walipe bondi ya milioni tatu ama dhamana ya pesa taslimu Sh300,000.

Hali kadhalika jaji Daniel Ogembo hata hivyo amewazuia sita hao dhidi ya kuenda katika eneo la Kianjokoma ambapo mauaji hayo yalitokea.

Hata hivyo mmoja wa washukiwa, Mputhia ambaye nyumbani kwake ni Meru ameruhusiwa kupitia Embu akielekea nyumbani .

Mnamo mwezi Septemba sita hao walikanusha mashtaka ya mauaji dhidi ya yao.

Upande wa mashtaka uliomba washukiwa wa kiume wazuiliwe katika gereza ya Industrial Area huku wale wa kiume wakizuiliwa katika gereza ya wanawake ya Lang'ata.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved