In Summary

•Habari njema ni kuwa  hakuna yeyote aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha katika mkasa huyo kwani tayari wanafunzi wote walikuwa madarasani kwa wakati huo.

Moto mkubwa
Image: WIKIPEDIA

Wanafunzi katika shule ya upili ya Kakamega wameamkia moto mkubwa ulioteketeza mabweni mawili.

Moto huo ambao unaripotiwa kuanza mwendo wa saa  kumi na mbili asubuhi uliteketeza malazi ya wanafunzi 584.

Habari njema ni kuwa  hakuna yeyote aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha katika mkasa huyo kwani tayari wanafunzi wote walikuwa madarasani kwa wakati huo.

Hata hivyo mali  yenye thamani kubwa isiyojulikana iliharibiwa na moto huo

Mwalimu mkuu wa shule hiy Gerald Orina amesema kwamba wanafunzi walijaribu kuuzima moto ule ila juhudi zao zote ziligonga mwamba.

Baadhi ya wazazi walifika pale shuleni baada yakupokea habari kuhusu moto uliokuwa umetokea.

Orina amehimiza wazazi walio na wanafunzi katika shule hiyo kuwa watulivu huku uchunguzi kuhusiana na chanzo cha moto ukiendelea.

Amesema kwamba bado hawajaweza kubaini kilichosababisha moto huo.

View Comments