In Summary
  • Hii leo hamna mtu ambaye ameaga dunia kutokana na coona huku idadi ya walioaga dunia ikisalia 5,312
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Kenya imesajili visa 20 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 3,136 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 19 ni wakenya huku1 akiwa ni raia wa kigeni,11 ni wanaume huku 9 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 253,853 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.6%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,741,836.

Vile vile watu 70 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,370,55 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 15 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hii leo hamna mtu ambaye ameaga dunia kutokana na coona huku idadi ya walioaga dunia ikisalia 5,312

Kuna wagonjwa 402 ambao wamelazwa hospitalini, 1,093 wamejitenga nyumbani.

Huku hayo yakijiri kuna wagonjwa 33 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,639,952.

 

 

 

 

View Comments