logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Moto wateketeza soko ya Gikomba kwa mara nyingine

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya mahakama kuruhusu huduma ya mji wa Nairobi (NMS) kufurusha baadhi ya wauzaji wa Mitumba katika soko ile ili kupatia nafasi upanuaji wa zahanati ya  Pumwani Majengo.

image
na SAMUEL MAINA

Habari08 November 2021 - 06:03

Muhtasari


  • •Moto huo uliteketeza mali ya mamilioni ya pesa katika soko hiyo kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashiriki.
  • •Haya yanajiri masaa machache tu baada ya mahakama kuruhusu huduma ya mji wa Nairobi (NMS) kufurusha baadhi ya wauzaji wa Mitumba katika soko ile ili kupatia nafasi upanuaji wa zahanati ya  Pumwani Majengo.
Moto wateketeza soko ya Gikomba Novemba 8, 2021

Wapelelezi na wataalamu wa moto wametumwa katika soko la Gikomba kuchunguza kisa kingine cha moto uliotokea usiku wa kuamkia Jumatatu.

Moto huo uliteketeza mali ya mamilioni ya pesa katika soko hiyo kubwa zaidi katika ukanda wa Afrika Mashiriki.

Polisi wanasema takriban ekari tatu za ardhi ambazo zilikuwa na vibanda na nguo zimeteketezwa na moto huo uliozuka mwendo wa  saa sita usiku.

Wafanyibiashara wachache tu ndio waliweza kuokoa mali yao kwani moto ule ulienea kwa kasi mno ukiteketeza kila kitu kilichokuwa katika eneo lililoathirika.

Chanzo cha moto huo bado hakijatambulika.

Haya yanajiri masaa machache tu baada ya mahakama kuruhusu huduma ya mji wa Nairobi (NMS) kufurusha baadhi ya wauzaji wa Mitumba katika soko ile ili kupatia nafasi upanuaji wa zahanati ya  Pumwani Majengo.

Moto huo umekuja wakati ambapo serikali iliahidi kuweka kamera za CCTV hapo kushughulikia matukio hayo ya mara kwa mara. Tukio kama hilo lilitokea mahali hapo mwezi uliopita. Hakuna aliyekamatwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved