In Summary
  • Kati ya maambukizi hayo 20 ni wakenya huku 1 akiwa ni raia wa kigeni,14 ni wanaume huku 7 wakiwa wanawake
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 11 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 77
Image: HISANI

Watu 21  wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 2,709 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 20 ni wakenya huku 1 akiwa ni raia wa kigeni,14 ni wanaume huku 7 wakiwa wanawake.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 11 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 77.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 254,297 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 0.8%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,770,062.

Aidha watu12 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 247,645,10 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 2 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Idadi ya watu walioaga inasalia kuwa  5,316kwani hamna mtu ambaye ameaga hii leo kutokana na corona.

Kuna wagonjwa 391 ambao wamelazwa hospitalini, 1,031 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 26 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 5,990,974.

 

 

 

Image: HISANI
View Comments