In Summary

•Afisa wa upelelezi wa uhalifu katika kaunti ya Kisumu Francis Wanjau alisema 18 waliandikisha taarifa na watafika kwenye kituo kila watakapohitajika.

•Mshukiwa alikabidhi keshia bahasha yenye barua iliyomwelekeza aweke noti za Sh1,000 tu.

Polisi wakabiliana na majambazi waliovamia benki Kisumu
Image: DAN OGENDO

Polisi katika kaunti ya Kisumu wameachilia huru watu 18 ambao walikamatwa kufuatia uvamizi wa benki ya Equity , tawi la Ang'awa siku ya Jumatatu.

Kumi na wanne kati ya walioachiliwa  ni wafanyikazi wa benki hiyo ilhali wanne ni wateja ikiwemo mhadhiri wa chuo kikuu.

Afisa wa upelelezi wa uhalifu katika kaunti ya Kisumu Francis Wanjau alisema 18 waliandikisha taarifa na watafika kwenye kituo kila watakapohitajika.

Wanjau alisema watahifashi simu zao ili kutumika katika uchunguzi zaidi.

Inamaanisha kufikia sasa hakuna aliyetiwa mbaroni.

Video ya CCTV inaonyesha mshukiwa mmoja akizungumza na keshia.

Mshukiwa alikabidhi keshia bahasha yenye barua iliyomwelekeza aweke noti za Sh1,000 tu.

Ujumbe mwingine ulisema "Kuna majambazi wanne katika benki waliojihami kwa bunduki, guruneti na visu"

Barua hiyo iko mikononi mwa DCI wa Kisumu ya kati David Sichangi ambaye anashughulikia kesi hiyo.

Mshukiwa huyo pia anaonekana akirusha gesi mtungi wa gesi ya machozi  kisha kutoa kofia na shati anapoondoka.

Kamera iliyokuwa kwenye kiingilio ilirekodi mshukiwa akiashiria kwa kutumia mkono wake. Anaonekana akitoroka kuelekea benki ya Oginga Odinga street.

Raia wamehoji jinsi polisi walimaliza operesheni hiyo. 

Uvamizi huo ulitokea mwendo wa saa tano unusu na kuendelea kwa masaa matatu.

(Utafsiri: Samuel Maina)

View Comments