In Summary

• Otieno alipokuwa anatoroka kuokoa maisha yake alitoa kisu chake na kukitumia kukata jirani yule kichwani kwa kuwaharibia 'sherehe' yao.

Crime scene photo

Polisi katika kaunti ya Nairobi wanazuilia mshukiwa mmoja wa wizi mabavu kufuatia tukio la ujambazi lililotokea katika nyumba moja mtaa wa Shauri Moyo.

Ian Otieno 25, na wenzake watatu walikuwa wamevamia nyumba ya familia katika eneo la Juakali mwendo wa saa nne usiku wa Jumanne na kuagiza wenye nyumba walale chini kabla ya kuiba simu tatu, runinga ya inchi 43 kati ya vitu vingine vya thamani.

Kwa bahati nzuri jirani mmoja aliwaona majambazi hao wakitishia familia ile na akaanza kupiga nduru ambayo iliwashtua wakaanza kutoroka.

Kulingana na DCI, Otieno alipokuwa anatoroka kuokoa maisha yake alitoa kisu chake na kukitumia kukata jirani yule kichwani kwa kuwaharibia 'sherehe' yao.

Mwenye nyumba iliyokuwa inavamiwa alipigia polisi kutoka kituo cha Shauri Moyo ambao walifuata genge lile na kuweza kumkamata Otieno akiwa bado amebeba televisheni ambayo  walikuwa wameiba.

Kisu kilichokuwa na damu kilipatikana kikiwa kimefichwa kwenye suruali yake.

Polisi wanaendelea kuwasaka wenzake Otieno huku akiwa anasubiri kufikishwa mahakamani.

View Comments