In Summary

Wawili hao, Mary Wambui Mungai na Purity Njoki Mungai pia walipuuza agizo la kufika mbele ya mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya (KRA). 

Hati ya kukamatwa ilitolewa dhidi ya wakurugenzi hao.

 

Mfanyabiashara Mary Wambui. Picha: KWA HISANI

Wakurugenzi wawili wa kampuni ya Purma Holdings limited walikosa kufika kortini siku Jumatatu kujibu mashtaka ya kutolipwa ushuru wa Shilingi bilioni 2.2. 

Wawili hao, Mary Wambui Mungai na Purity Njoki Mungai pia walipuuza agizo la kufika mbele ya mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya (KRA). 

Wawili hao walipaswa kushtakiwa kwa makosa manane ya kukwepa kulipa kodi makusudi kuambatana na stakabadhi za ushuru wa mapato zilizowasilishwa kwa Kamishna wa Kodi ya Ndani kwa kipindi cha kati ya mwaka 2014 - 2016. 

Hati ya kukamatwa ilitolewa dhidi ya wakurugenzi hao. Hakimu wa Mahakama dhidi ya ufisadi, Felix Kombo alisema upande wa mashtaka uliwasilisha nakala za nyaraka kuonyesha washtakiwa walipewa hati za wito. 

Hii ilitokana na madai ya upande wa utetezi kuwa wateja wao hawakupewa hati za wito. Upande wa utetezi ulidai Wambui amelazwa katika Hospitali ya Nairobi tangu Novemba 29, na hakuweza kuhudhuria korti. 

Waliomba siku 10 kuwasilisha Njoki kwa vile hakupewa hati za wito. Dhamana ya kutarajia waliyoomba mbele ya Mahakama Kuu jijini Nairobi mnamo Desemba 3 ilifeli kwani hakuna mwelekeo uliotolewa. 

Upande wa mashtaka ulipinga ombi hilo na ulisema hakuna rekodi za matibabu zilizowasilishwa kuthibitisha madai hayo. 

"Ni wazi wakurugenzi walikabidhiwa wito na washtakiwa walikabidhiwa stakabadhi za wito ipasavyo na walipuuzwa kufika," alisema hakimu.

View Comments