In Summary

•Seneta huyo amemtaja  marehemu kama mama mkwe mpole na kiongozi  wa familia aliyependa kudumisha maadili.

Gideon Moi
Image: MAKTABA

Mama mkwe wa seneta wa Baringo Gideon Moi ameaga dunia.

Gideon ametangaza kuhusu kifo cha mama ya mkewe Zahra Moi  na kumuomboleza kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Katika ujumbe wake wa rambirambi, Seneta huyo amemtaja  marehemu kama mama mkwe mpole na kiongozi  wa familia aliyependa kudumisha maadili.

"Nimehuzunika sana asubuhi ya leo kwa kufiwa na Mama Afia Juma - mama ya mke wangu mpendwa Zahra Moi. Mama mkwe mpole, Mama Afia Juma alikuwa ni mnyenyekevu, mtambuzi wa kina lakini kiongozi wa familia mkali sana" Gideon alisema.

Gideon amesema kifo cha Bi. Afia  ni pigo kubwa kwa familia huku akiomba Mola awajalie nguvu ya kupambana na majonzi kufuati msiba uliowapata ghafla.

"Kifo chake ni pigo kubwa kwetu kama familia. Mwenyezi Mungu atujalie neema ya kutosha katika kipindi hiki kigumu ili tuweze kukabiliana na msiba huu" Ameandika Gideon.

Katibu mkuu wa chama cha KANU Nick Salat  ametangaza Mama Afia Juma alifariki asubuhi ya Alhamisi.

Chama hicho kimemwomboleza mama mkwe wa mwenyekiti wao huku kikitakia familia nguvu ya kustahili majonzi yaliyowakumba.

"Kifo cha Mama Afia Juma, mama mzazi wa Zahra Moi ambaye ni mke wa Mwenyekiti wetu Taifa, mapema leo hakika ni jambo la kuhuzunisha sana. Kama chama, tunatuma risala zetu za rambirambi na kuwahakikishia kuwa ziko katika mawazo na maombi yetu katika kipindi hiki kigumu. Mwenyezi Mungu ampe Zahra Moi na familia nzima ujasiri wa kustahimili msiba huo." Ujumbe wa Salat ulisoma.

View Comments