In Summary
  • Mswada wa vyama waahirishwa na naibu Spika
  • Cheboi akizungumza alisema kutokana mapendekezo yaliyoletwa lazima kwanza yashughulikiwe
Wabunge wa Bunge la Kitaifa na Seneti wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11
Image: FILE

Naibu wa Spika  Moses Cheboi Jumatano aliahirisha maswada ulioletwa Bungeni na kiongozi wa wengi Amos Kimunya kujadiliwa kwa hatua ya tatu.

Cheboi aliagiza kamati  yake ya sheria kushughulikia pendekezo zilizoletwa na wabunge hasa wa kutoka mrengo wa naibu raisi ambazo zilikuwa taribani 20.

Mswada huo ambao ulipita hatua mbili za sheria, na kubakisha moja. Uliahirishwa kufuatia ongezekeko la mapendekezo ya kuufanyia marekebisho yaliyowashiliishwa Bungeni.

Cheboi akizungumza alisema kutokana mapendekezo yaliyoletwa lazima kwanza yashughulikiwe.

Kiongozi wa wengi Amos Kimunya  alieleza imani yake kwa mswada huo, huku akisema ako na hakika mswada utapita kwenye hatua iliyosalia bila marekebisho yoyote  

KIongozi wa wachache John  Mbadi akimulaumu naibu spika  kwa kuwa na maegemeo licha ya pande yao kushinda kwa kura 113 dhidi 68 baada ya mswada huo kusomwa mara ya pili alisisitiza hatua hio ni kinyume nataratibu ya bunge 

"Imedhirika wazi tuko na wabunge wengi bungeni, isikuwe kizingizio sasa, kama mlikuwa na shaka nadhani mmeona,...kusema hayo spika akufanya maamuzi  sawa  ikizingatiwa shughuli hii ndiyo ilituleta hapa kujadili ....na kwa sababu spika ndiye mwenye usemi mkubwa, hakuna kitu tunaweza fanya".

Wabunge wa merngo wa naibu rais waliimba na kushangilia  kufuatia maamuzi ya naibu spika na kusema hio ilikuwa mbinu yao ya kuhakikisha mswada huo hujapita  hatua hio.  

 

View Comments