In Summary
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 310,797 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 19.2%
  • Mgonjwa wa chini ana umri wa mwezi 1 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 110
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,094,153
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Visa 1,667 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini  siku ya JUmamosi kutoka kwa sampuli 8,703 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 1,462 ni wakenya huku 205 wakiwa raia wa kigeni,840 ni wanaume huku 827 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 310,797 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 19.2%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa mwezi 1 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 110.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,094,153.

Vile vile watu 2,523 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 264,656, 2,395 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 128 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 12 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,437

Kuna wagonjwa 1,210 ambao wamelazwa hospitalini, 25,991 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 54 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,572,187.

 

 

 

 

View Comments