In Summary

•Msichana huyo alifariki kutokana na maradhi yaliyohusiana na unyanyasaji wa kingono baada ya kunajisiwa na mshtakiwa ambaye ni mjomba wake.

•Mwalimu wa mtoto huyo aligundua kwanza kwamba msichana alikuwa na shida ya kutembea na alijitenga na wenzake wa rika moja.

•Kwa kuhofia maisha yake msichana huyo  baadaye alitoweka nyumbani mnamo Julai 2021 na kuishi msituni kwa siku tano hivyo kuzua hofu miongoni mwa wanakijiji.

Haron Cherono, 60, aliyeshtakiwa kwa kumnajisi mpwa wake wa miaka 10 alihukumiwa kifungo cha maisha katika mahakama ya sheria ya Kabarnet, Baringo mnamo Jumanne, Januari 11, 2022
Image: JOSEPH KANGOGO

Mzee mmoja wa miaka 60 kutoka Baringo ambaye alimnajisi msichana wa miaka 10 na kusababisha kifo chake amehukumiwa kifungo cha maisha.

Mnamo Jumanne Hakimu Mkuu wa Kabarnet Judy Wanjala alimpata mshtakiwa Haron Cherono na hatia ya kuua bila kukusudia.

"Sidhani kama kuna adhabu nyingine ya kuua bila kukusudia chini ya kifungu cha 205 cha kanuni ya adhabu ila kifungo cha maisha," Wanjala alisema.

Msichana huyo alifariki kutokana na maradhi yaliyohusiana na unyanyasaji wa kingono baada ya kunajisiwa na mshtakiwa ambaye ni mjomba wake.

Kufikia kifo chake marehemu alikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu. Aliugua kutokana na kisa hicho cha ubakaji na baadaye akafa akiwa katika makao ya watoto ya Kabarnet Sunrise, Kaunti Ndogo ya Baringo ya Kati mnamo Julai 24, 2021.

Katika uamuzi wake, Wanjala alisema alizingatia hali ambayo uhalifu huo ulitekelezwa. Aliongeza kuwa umri wa mwathiriwa pia ni suala la maslahi ya umma.

"Hii itakuwa kama funzo kwa wale wanaonajisi watoto wadogo, wanapaswa kujua bila shaka watakabiliwa na nguvu kamili ya sheria," alisema.

Alisema chini ya kifungu cha 8 (1) cha makosa ya kingono, iwapo mtoto hangefariki, basi mhalifu angeshtakiwa kwa kosa la unajisi.

Inasemekana kwamba mzee huyo ni mume wa shangazi wa msichana huyo.

Kulingana na madaktari, maambukizi hayo baadaye yalisababisha maambukizo ya bakteria na virusi katika mfumo wa uzazi  wa marehemu, hali ambayo hayakutambuliwa na kutibiwa mapema.

"Marehemu alikuwa amevimba upande wa chini wa miguu. Hatimaye alifariki baada ya figo yake kushindwa kufanya kazi,” mtaalamu wa magonjwa ya Serikali Dkt Wangare Wambugu alisema

Alisema alipouchunguza mwili wa marehemu ambao ulikuwa ukioza mnamo Agosti 3, 2021 aligundua kwamba figo zake zote mbili zilikuwa zimeharibika sana, hali ambayo ingeweza kusababisha kifo cha mapema.

Mwalimu wa mtoto huyo aligundua kwanza kwamba msichana alikuwa na shida ya kutembea na alijitenga na wenzake wa rika moja.

"Baada ya kuhojiwa, alinifichulia kwa siri kwamba hakika mjomba wake alikuwa akimnyanyasa kingono mara kwa mara," alisema.

Msichana huyo alisema mjombake alikuwa akimpa sarafu za shilingi kumi au tano na kutishia kumuua iwapo angethubutu kuripoti kisa hicho kwa mtu yeyote.

Kwa kuhofia maisha yake msichana huyo  baadaye alitoweka nyumbani mnamo Julai 2021 na kuishi msituni kwa siku tano na hivyo kuzua hofu miongoni mwa wanakijiji.

Baada ya kutafutwa kwa muda mrefu, alipatikana akiwa mgonjwa sana, mwenye njaa na dhaifu. Alikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti-Kabarnet na kisha kuhamishwa mara moja hadi Hospitali ya Kufundisha na Rufaa ya Moi (MTRH)-Eldoret.

Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini, idara ya watoto ya kaunti hiyo baadaye ilipendekeza mgonjwa huyo auguzwe chini ya ulinzi salama kisha akapelekwa katika nyumba ya watoto ya Kabarnet sunrise ambapo hali yake ilizidi kuwa mbaya na akafa mnamo Julai 24, 2021, mida ya usiku wa manane.

View Comments