In Summary

• Mimea hiyo ni mali ya wanaharakati kutoka jamii ya wazawa ya Khoisan, ambao baadhi yao wamekita kambi katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka mitatu.

AFP
Image: AFP

Mfalme wa Khoisan wa Afrika Kusini  akamatwa kwa kupanda bangi katika ofisi ya rais.

Mimea hiyo ni mali ya wanaharakati kutoka jamii ya wazawa ya Khoisan, ambao baadhi yao wamekita kambi katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kiongozi wao, ambaye hujiita Mfalme wa Khoisan, alianguka ndani ya mmea wa bangi wakati polisi walipokuwa wakimburuza kumlazimisha atoke wamkamate na kumpeleka kituo cha polisi.

"Polisi ... mmetangaza vita?," shirika la habari la AFP lilimnukuu Mfalme wa Khoisan akipaza sauti akisema.

"Tumekuwa hapa kwa amani. Tunawajia," aliendelea. Baada ya matamshi hayo alikamatwa.

Yeye na baadhi ya wanaharakati waliokamatwa kwa "kuhusika na dagga (bangi), upandaji na uvunaji haramu wa bangi na kukataa kuvaa barakoa wanapokuwa katika maeneo ya umma wakati walipoamrishwa na afisa wa polisi kufanya hivyo," taarifa ya AFP ilisema.

AFP
Image: AFP

Mnamo mwaka 2018, kikundi hicho kiliweka kambi yao katika eneo la bustani nje ya ofisi ya rais, karibu na sanamu kubwa ya Nelson Mandela, kufanya kampeni ya kutambuliwa rasmi kwa lugha yao.

Mke wa Mfalme wa Khoisan ameelezea kukasirishwa kwake na tukio hilo katika mahojiano na wavuti wa habari wa Afrika Kusini wa IOL.

View Comments