In Summary
  • Visa 1,035 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 9,337 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo 8559 ni wakenya huku 176 wakiwa raia wa kigeni,566 ni wanaume huku 469 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 316,700 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 11.1%
Image: HISANI

Visa 1,035 vipya vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 9,337 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 8559 ni wakenya huku 176 wakiwa raia wa kigeni,566 ni wanaume huku 469 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 316,700 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 11.1%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 3 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 110.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,136,817.

Vile vile watu 1,155 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 280,199, 1,042 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 113 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Kwa habari za kuhuzunisha Watu 10 wameaga dunia kutokana na corona huku idadi ya walioaga ikifika 5,482.

Kuna wagonjwa 1,119 ambao wamelazwa hospitalini, 14,791 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 48 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 10,974,305.

 

 

 

 

 

View Comments