In Summary

• Polisi waliwatawanya kundi la vijana waliokuwa wamesafirishwa hadi nje ya ofisi ya mfanyabiashara Jimi Wanjigi. 

• Wanjigi alisema tukio hili limechochewa kisiasa kutokana na msimamo wake na hasa matamshi aliyotoa wikendi. 

• Baada ya kuingia katika eneo hilo, maafisa hao wenye silaha waliripotiwa kukataa kuwahutubia mawakili wake na badala yake wakaamuru aandamane nao ili kurekodi

Polisi watawanya kundi la vijana waliokuwa wamesafirishwa hadi nje ya ofisi ya mfanyabiashara Jimi Wanjigi. Picha: CYRUS OMBATI

Polisi waliwatawanya kundi la vijana waliokuwa wamesafirishwa hadi nje ya ofisi ya mfanyabiashara Jimi Wanjigi. 

Wengine walikuwa wamefika ndani ya mabasi matatu na kabla ya wale waliokuwemo kushuka, gesi za kutoa machozi zilipigwa na kuwalazimisha madereva kuondoka kwa kasi. 

Polisi walisema baadhi ya waliokuwa katika kundi hilo walikuwa wakiwaibia wananchi waliokuwa wakitembea kwa miguu na madereva wa magari. 

Wanjigi alikuwa bado amejificha ndani ya ofisi yake kufikia saa nne unusu asubuhi. 

Polisi kutoka DCI Kitengo cha Kupambana na Ugaidi wamekita kambi katika ofisi za Wamjigi tangu Jumatatu usiku. 

Image: Mercy Mumo

Walisema walitaka Wanjigi arekodi taarifa kuhusu uchunguzi wanaofanya kuhusiana na kipande cha ardhi mtaani Westlands. 

Wanjigi alisema tukio hili limechochewa kisiasa kutokana na msimamo wake na hasa matamshi aliyotoa wikendi. 

“Walijaribu hili mwaka wa 2017 na wakafeli… Ni mchezo sawa wanajaribu kunitisha. Baadhi ya watu hawapendezwi na siasa zangu au jinsi ninavyozungumza… nasema tu ukweli na sidhani kama kuna ubaya kusema ukweli,” aliongeza. 

Kuhusu kile kilichojiri wakati wa uvamizi huo, Wanjigi alisema maafisa wa upelelezi wa DCI walifika katika afisi zake za Kwacha Group of Companies huko Westlands, Nairobi na kutaka kumuona binafsi. 

Baada ya kuingia katika eneo hilo, maafisa hao wenye silaha waliripotiwa kukataa kuwahutubia mawakili wake na badala yake wakaamuru aandamane nao ili kurekodi taarifa bila kufichua suala hilo lilihusu nini.

View Comments