In Summary
  • Kati ya maambukizi hayo 71 ni wakenya huku 20 wakiwa raia wa kigeni,51 ni wanaume huku 40 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 320,229 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.8%
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,186,286
Image: HISANI

Visa 91 vya maambukizi ya corona vimerekodiwa nchini kutoka kwa sampuli 3,229 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 71 ni wakenya huku 20 wakiwa raia wa kigeni,51 ni wanaume huku 40 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 320,229 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.8%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,186,286.

Vile vile watu 1,814 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 291,361, 1,676 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 138 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 23 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,554.

Kuna wagonjwa 746 ambao wamelazwa hospitalini, 6,011 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 40 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 11,542,128.

 

 

 

 

 

View Comments