In Summary
  • Watu 2 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,567
  • Kuna wagonjwa 569 ambao wamelazwa hospitalini, 5,178 wamejitenga nyumbani
  • Vile vile kuna wagonjwa 21 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MAKTABA

Watu 152 wamepatikana na maambukizi ya corona nchini kutoka kwa sampuli 5,666 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 131 ni wakenya huku 21 wakiwa raia wa kigeni,87 ni wanaume huku 65 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 320,918 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.8%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,206,603.

Vile vile watu 430 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 293,017, 348 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 82 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 2 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,567.

Kuna wagonjwa 569 ambao wamelazwa hospitalini, 5,178 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 21 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 11,784,132.

 

 

 

 

View Comments