In Summary
  • Watu 4 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,587
  • Kuna wagonjwa 413 ambao wamelazwa hospitalini,4,545 wamejitenga nyumbani
  • Vile vile kuna wagonjwa 10 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU)
Waziri wa afya Mutahi Kagwe
Image: Mercy Mumo

Watu 171 wamepatikana na maambukizi ya corona nchini kutoka kwa sampuli 6,137 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 131 ni wakenya huku 40 wakiwa raia wa kigeni,82 ni wanaume huku 89 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 321,552 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.8%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,229,023.

Vile vile watu 137 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 294,859, 112 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 25 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 4 wameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona huku idadi hiyo ikifika 5,587.

Kuna wagonjwa 413 ambao wamelazwa hospitalini,4,545 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 10 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 12,451,246.

 

 

 

 

 

 

View Comments