In Summary

• Mbunge wa Kajiado kaskazini, Peris Tobiko Jumanne alipata kipindi kigumu kuzungumza na wakazi wa eneo la Kimama kuwaomba kura za ugavana kaunti ya Kajiado wakati ambapo wananchi hao walimpigia kelele bila kumpa nafasi ya kuzungumza.

• Mbunge huyo alijaribu kuutuliza umati huo ulioonekana kuwa na kero bila mafanikio, huku akipigiwa kelee na wale waliodhaniwa kuwa wafuasi wake Katoo.

Mbunge wa Kajiado kaskazini, Peris Tobiko Jumanne alipata kipindi kigumu kuzungumza na wakazi wa eneo la Kimama kuwaomba kura za ugavana kaunti ya Kajiado wakati ambapo wananchi hao walimpigia kelele bila kumpa nafasi ya kuzungumza.

Peris Tobiko alikuwa amepishwa kuzungumza na mpinzani wake katika kinyang’anyiro hicho, Katoo Ole Metito, ambapo alikutana na majembe ya wafuasi waliowakaribisha ambao walionekana kutoufurahia uwepo wake kwenye mkutano huo.

Mbunge huyo alijaribu kuutuliza umati huo ulioonekana kuwa na kero bila mafanikio, huku akipigiwa kelee na wale waliodhaniwa kuwa wafuasi wake Katoo.

Naibu rais William Ruto ambaye alikuwa katika mkutano huo alitazama ‘sinema’ hiyo bila usaidizi wowote ule.

 “Nyinyi mumesema hiyo yenu Katoo, na nikimshinda Katoo? mtanipatia hiyo kura? (I can see you have endorsed Katoo, what if I beat him? Will you vote for me?)?” Tobiko alisaili.

Mrengo wa Kenya kwanza ulikita kambi katika kaunti hiyo ya Kajiado ili kusaka uungwaji mkono mbele ya uchaguzi mkuu unaoratibiwa kufanyika tarehe 9/8/2022, huku Peris Tobiko akiwa miongoni mwa viongozi walioandamana na William Ruto, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula katika kampeni hizo.

Tobiko na Katoo wanawania ugavana wa kaunti hiyo kupitia chama cha UDA huku ikisubiriwa kuona nani ataibuka kidedea katika kura za mchujo chamani humo.

Awali akizungumza na wakazi, Katoo aliwaomba watu wote kudumisha amani na kuwakaribisha wagombea wote ili wauze sera zao, na kusema kwamba yupo tayari kutoana kijasho na Tobiko katika kura za mchujo na kuwa atamuunga mkono yeyote atayeshinda kura hizo.

 

View Comments