In Summary

Daraja lililojengwa na serikali ya kaunti ya Kajiado kwa kiasi cha shilingi milioni mia moja limeanguka wiki moja tu baada ya kuzinduliwa rasmi na gavana Joseph Ole Lenku .

Ole lenku aliongezea kwamba kero la malori kukwama katika mto Olkeriai katika vipindi vya mvua nyingi, lingemalizwa na daraja hilo.

sigiri2

Daraja lililojengwa na serikali ya kaunti ya Kajiado kwa kiasi cha shilingi milioni mia moja limeanguka wiki moja tu baada ya kuzinduliwa rasmi na gavana Joseph Ole Lenku .

Kulingana na wakazi wa eneo hilo, daraja hilo lilianguka kutokana na mvua nyingi inayoshuhudiwa katika kaunti hiyo, huku wakiongezea kwamba nguzo za daraja hilo zilizosalia zinaonekana kulegea.

Kulingana na serikali ya kaunti ya Kajiado, daraja hilo liligharimu shilingi milioni mia moja kutengenezwa na kufunguliwa  rasmi kwa wananchi kutumia mnamo tarehe 17/2/2022 na gavana  wa kaunti ya Kajiado, Joseph Ole Lenku.

Awali katika uzinduzi wake, Ole Lenku alisifu mradi huo huku akisema kwamba alisema daraja hilo lingefungua na kuboresha biashara ya maua katika eneo hilo na pia kumaliza changamoto zinazoletwa na mvua ambazo huwapa wachuuzi kipindi kigumu kusafirisha bidhaa zao.

“Daraja hili linasaidia usafirishaji wa vyakula katika eneo la Kajiado mashariki, kajiado ya kati na kusini huku wanaofaidi pakubwa wakiwa wakulima kutoka vijiji vya Eselenkei, Emashini, IItuleta, Olanti Mashuuru, na  Lenkisim ,” gavana huyo aliandika katika ukurasa wake wa Facebook.

Ole lenku aliongezea kwamba kero la malori kukwama katika mto Olkeriai katika vipindi vya mvua nyingi, lingemalizwa na daraja hilo.

View Comments