In Summary

• Mwanaume mmoja , 35 Jumatano usiku alishambuliwa na kuawa na fisi katika kijiji cha Juja kilichopo kaunti ya Kiambu.

• Kisa hiki kinajiri miezi miwili tu baada ya watu wengine wawili kushambuliwa na kuawa na fisi hao waliokuwa wanazurura katika maeneo ya Witeithie na Thika.

hyena

Mwanaume mmoja , 35 Jumatano usiku alishambuliwa na kuawa na fisi katika kijiji cha Juja kilichopo kaunti ya Kiambu.

Duru za kuaminika zinasema kwamba, Robert Mwangi alisikika akipiga kamsa na kuomba usaidizi karibia saa saba usiku.

Majirani walikimbia na kufika katika eneo la mkasa ila hawangeweza kumuokoa kutoka kwa midomo ya fisi nane waliokuwa wamemshambulia.

Chifu wa eneo hilo, Sarah Wanjiku alithibitisha kisa hicho na kusema kwamba familia ya marehemu ilikuwa imejulishwa kuhusu shambulizi hilo, na baadaye mwili wa Mwangi ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya General Kago iliyopo mjini Thika.

Kisa hiki kinajiri miezi miwili tu baada ya watu wengine wawili kushambuliwa na kuawa na fisi hao waliokuwa wanazurura katika maeneo ya Witeithie na Thika.

Mwishoni mwa mwaka jana, polisi kupitia idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI iliwaonya wakazi wa maeneo ya Juja na Thika kuhusu wanyama hao ambao walikuwa wakiwahangaisha wakazi.

 

View Comments