In Summary

• Maafisa wa afya katika kaunti ya Mombasa wametoa notisi ya siku saba walipwe mishahara yao ama washiriki mgomo.

• Maafisa hao wanasema kwamba licha ya juhudi zao za muda mrefu, serikali ya kaunti haijachukua hatua yoyote ya kutekeleza matakwa yao.

KWA HISANI
Image: STAR

Maafisa wa afya katika kaunti ya Mombasa wametoa notisi ya siku saba walipwe mishahara yao ama washiriki mgomo.

Maafisa hao wanasema kwamba licha ya juhudi zao za muda mrefu, serikali ya kaunti haijachukua hatua yoyote ya kutekeleza matakwa yao.

Kupitia kwa taarifa ya pamoja iliyotolewa na miungano ya wafanyikazi siku ya jumatatu, maafisa hao wa afya walisema kwamba wanataka walipwe mishahara yao ya miezi ya Januari na Februari ili waweze kurejelea majukumu yao ya kawaida.

“Tunataka kusema kwamba licha ya juhudi zetu za kufanya mazungumzo na serikali ya kaunti ya Mombasa na washikadau wote ili kushughulikia matakwa yetu, uongozi wa kaunti umepuuza malalamishi yetu huku mishahara yetu ikicheleweshwa,” taarifa hiyo ilisoma.

  Licha ya kutishia kugoma, maafisa hao wa afya wamesema kwamba wapo radhi kufanya mazungumzo na serikali ya kaunti ya Mombasa ili kutatua zogo hilo.

 

View Comments