In Summary

• Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ameunga mkono hatua ya Urusi kushambulia Ukraine.

• Anakuwa kiongozi wa kwanza kutoka bara la Afrika kusimama upande wa Urusi.

KWA HISANI
Image: Muhoozi Kainerugaba

Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni Kamanda wa Majeshi ya Nchi kavu ya Uganda ametoa kauli ya kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika “…Watu wengi (ambao sio Wazungu) wanaunga mkono msimamo wa Urusi nchini Ukraine, Putin yuko sahihi kabisa."

"Wakati USSR ilipoweka makombora yenye silaha za nyuklia nchini Cuba mwaka 1962, Nchi za Magharibi zilikuwa tayari kulipua ulimwengu juu yake, sasa NATO ikifanya hivyo wanatarajia Urusi kufanya tofauti!?"Muhoozi aliandika.

Jenerali Kainerugaba ndiye Afisa Mkuu wa Kwanza wa Kijeshi Afrika kuunga mkono hadharani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Jenerali huyo anatajwa kuwa anaweza kuwa Rais wa Uganda katika siku za usoni na kumrithi Baba yake mwenye umri wa miaka 77 ambaye amekuwa madarakani tangu 1986.

View Comments