In Summary

• Wakili Makau Mutua amesema kwamba kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka hawezi kutoa upinzani wowote kwa  Raila Odinga, iwapo watawania kiti cha urais kutumia tikiti moja.

• “Odinga anamzidi Kalonzo kiumri, na hivyo anapaswa kumuunga mkono. Naamini Kalonzo anajua hilo na haliwezi kubadilika,” Makau alisema.

 

Makau Mutua

 

Wakili Makau Mutua amesema kwamba kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka hawezi kutoa upinzani wowote kwa  Raila Odinga, iwapo watawania kiti cha urais kutumia tikiti moja.

Mutua ambaye ni msemaji wa jopokazi linalosimamia kampeni za Odinga, alisema kwamba kiongozi huyo wa ODM na muungano wa Azimio ana umaarufu mkubwa kote nchini na hivyo basi Musyoka anapaswa kutupilia mbali azma yake na kumuunga mkono Raila Odinga katika uchaguzi wa Agosti 9.

Aliongezea kuwa uchaguzi wa urais utakuwa na wagombeaji wawili wakuu : Raila Odinga na naibu rais William Ruto na kwamba Kalonzo hana nafasi katika kinyang’anyiro hicho.

“Odinga anamzidi Kalonzo kiumri, na hivyo anapaswa kumuunga mkono. Naamini Kalonzo anajua hilo na haliwezi kubadilika,” Makau alisema.

Kwa upande wa wakili huyo, anaamini kwamba Kalonzo bado ana miaka mingi ya kuwania kiti hicho.

Vilevile Makau Mutua alisema kwamba kiongozi huyo wa eneo la Ukambani amepoteza umaarufu na kwamba kwa sasa anapaswa kuzingatia kutafuta ushawishi wake katika eneo hilo.

Aidha Makau alimtaka Kalonzo kuungana na magavana wa ukambani Charity Ngilu, Alfred Mutua na Kivutha Kibwana katika mchakato wa kumuunga mkono Raila Odinga.

 

 

View Comments