In Summary

• Naibu rais William Ruto amesema kwamba wakili na mwanaharakati, Miguna Miguna ataruhusiwa kurejea nchini iwapo atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa Agosti 9.

• “Tutamrudisha Miguna nyumbani kwa kipindi kifupi nikiwa rais,” Ruto alisema.

Naibu rais William Ruto
Image: DPPS

Naibu rais William Ruto amesema kwamba wakili na mwanaharakati, Miguna Miguna ataruhusiwa kurejea nchini iwapo atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi wa Agosti 9.

Miguna amekuwa nchini Canada tangu mwaka wa 2018 baada ya kushiriki katika shughuli ya kumuapisha Raila Odinga kama ‘rais wa wannachi.’

Kulingana na Ruto, Miguna ni mkenya na kwamba iwapo alifanya makosa yoyote basi anapaswa kukabiliana na sheria na wala sio kufurushwa.

“Tutamrudisha Miguna nyumbani kwa kipindi kifupi nikiwa rais,” Ruto alisema.

“Hii ni Kenya hata kama alifanya kosa, nchi hii ina sheria ambazo zinafanya kazi. Sioni haja ya kuwa na wakambizi ambao wanaishi katika taifa letu huku wakenya wenzutu wamefurushwa na wanaisha katika mataifa ya kigeni,” Ruto aliongezea.

Kauli hiyo ya naibu rais ilijiri wiki mbili tu baada ya Miguna kutangaza rasmi kwamba atakuwa anawania wadhfa wa ugavana katika kaunti ya Nairobi katika uchaguzi mkuu ujao. Wakili huyo mwenye misimamo mikali anashikilia kwamba yeye ni mkenya na ana kila haki ya kuwania nafasi yoyote anayoitaka.

“Ninakusudia kuwania kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi. Nimesajiliwa kama mpigakura na hivyo ninaweza kuwania cheo chochote,” Miguna alisema.

Aidha aliongeza kwamba hatakuwa anawania cheo hicho kama mgombea huru na kwamba atatangaza chama atakachokitumia hivi karibuni.

 

View Comments