In Summary

•Waendesha bodaboda wanaotoa huduma katika kaunti ya Nairobi hata hivyo hawajaponea kwani polisi bado wataendelea na msako mkali katika eneo la CBD.

Bodabodas
Image: MAKTABA

Msemaji wa polisi Bruno Shioso ametangaza kusitishwa kwa operesheni ya kitaifa ambayo imekuwa ikilenga wahudumu wa bodaboda.

Kupitia taarifa iliyotolewa Jumamosi, Shioso amesema uamuzi huo umefanywa ili kuepusha kuvuruga huduma zinazotolewa na waendeshaji wanaozingatia sheria.

Waendesha bodaboda wanaotoa huduma katika kaunti ya Nairobi hata hivyo hawajaponea kwani polisi bado wataendelea na msako mkali katika eneo la CBD.

"“Utekelezaji wa kufuata sheria za trafiki na pikipiki za uchukuzi wa umma almaarufu Boda boda umesitishwa. Hii ni kutoa nafasi kwa serikali kupanga upya sekta hii kupitia kamati ya sekta mbalimbali inayoshughulikia mfumo wa utekelezaji," Taarifa hiyo ilisoma.

Rais Uhuru Kenyatta aliamuru msako mkali katika sekta ya bodaboda nchini kufuatia kisa cha kutisha ambapo waendesha bodaboda walimnyanyasa kijinsia dereva wa kike katika barabara ya Wangari Maathai jijini Nairobi.

Wizara ya Masuala ya Ndani ilitoa msururu wa hatua za kusaidia kudhibiti sekta hiyo ambayo mara nyingi imehusishwa na ukora. Hatua hizo zitatekelezwa ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo.

View Comments