In Summary

•Kinara wa ODM, Raila Odinga ni miongoni mwa mashabiki sugu wa Arsenal ambao walifika Emirates kushuhudia mechi hiyo ikichezwa moja kwa moja.

•Hapo awali Raila alikuwa amebashiri kuwa timu yake ingepiga Liverpool 2-0 ila matokeo ya mechi hiyo yakawa kinyume.

Raila Odinga ashuhudia Wanabunduki wakicheza Emirates mnamo Machi 16, 2022
Image: TWITTER// RAILA ODINGA JR

Usiku wa Jumatano klabu ya Arsenal ilikaribisha mabingwa wa EPL msimu wa 2019-2020, Liverpool ugani Emirates.

Maelfu ya mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za dunia walitazama moja kwa moja Wanabunduki wakizimwa 0-2 na vijana wa Jurgen Kloop katika mechi yao ya 27 msimu huu huku maelfu wengine wakifuatilia mechi hiyo kwenye runinga zao.

Kinara wa ODM, Raila Odinga ni miongoni mwa mashabiki sugu wa Arsenal ambao walifika Emirates kushuhudia mechi hiyo ikichezwa moja kwa moja.

Raila alikuwa ameandana na wanawe wawili  Raila Odinga Jr na Winnie Odinga pamoja na viongozi wengine wa vuguvugu la Azimio la Umoja  wakiwemo gavana Hassan Joho, Seneta James Orengo, mbunge Junet Mohammed, Francis Atwoli na Peter Kenneth.

- Raila Odinga ashuhudia Wanabunduki wakicheza Emirates mnamo Machi 16, 2022
- Raila Odinga ashuhudia Wanabunduki wakicheza Emirates mnamo Machi 16, 2022
- Raila Odinga ashuhudia Wanabunduki wakicheza Emirates mnamo Machi 16, 2022

Hapo awali Raila alikuwa amebashiri kuwa timu yake ingecharaza Liverpool 2-0 ila matokeo ya mechi hiyo yakawa kinyume.

Arsenal imecheza dhidi ya Liverpool mara nne msimu huu na kukosa kufunga bao lolote katika mechi zote. Liverpool imewafunga mabao nane katika kipindi hicho.

View Comments