In Summary

•Kamishna wa Kaunti ya Uasin Gishu, Stephen Kihara viongozi wakuu wa kisiasa katika eneo hilo wamehusishwa kupanga tukio hilo.

•Huduma ya Kitaifa ya Polisi ilisema waliokamatwa walipatikana na manoti ya shilingi 50 na wanasaidia katika uchunguzi.

Ndege ya Raila Odinga ilishambuliwa kwa mawe katika kaunti ya Uasin Gishu Ijumaa
Image: FACEBOOK// RAILA ODINGA

Washukiwa 17 waliokamatwa kwa kushambulia ndege ya Raila Odinga watajibu mashtaka manne yakiwemo;  jaribio la mauaji, uharibifu wa mali na uchochezi.

17 hao walikamatwa Jumamosi kwa kuipiga mawe chopa ya mgombea urais wa Azimio la Umoja Raila Odinga katika eneo la Kabenes, kaunti ya Uasin Gishu baada ya mazishi ya Mzee Jackson Kibor.

Kamishna wa Kaunti ya Uasin Gishu, Stephen Kihara alisema waliokamatwa wametoa taarifa zaidi  kuhusiana na tukio hilo.

Aliongeza kuwa viongozi wakuu wa kisiasa katika eneo hilo wamehusishwa kupanga tukio hilo.

Kupitia taarifa, Huduma ya Kitaifa ya Polisi ilisema waliokamatwa walipatikana na manoti ya shilingi 50 na wanasaidia katika uchunguzi.

Kukamatwa huko kulijiri baada ya Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i kuagiza polisi kuchunguza na kuwakamata vijana waliohusika katika tukio hilo lililotokea Ijumaa.

Mengine yatafuata...

View Comments