In Summary
  • Siku ya Jumanne, Gedi alikariri kwamba ana ushahidi wa kuunganisha DP na madai ya unyakuzi wa ardhi
Image: Ezekiel Aming'a

Mwakilishi wa Wanawake wa Wajir, Fatuma Gedi, amewasilisha mfuko uliojaa ushahidi anaodai kumhusisha Naibu Rais William Ruto katika kesi za unyakuzi wa ardhi.

Akizungumza na wanahabari  mnamo Alhamisi, Aprili 14, Gedi alisema kuwa alikuwa tayari kuwasilisha ushahidi huo mbele ya ukumbi wa Bunge kwa mjadala.

Mwakilishi  huyo wa wanamke wa Wajir alidokeza kwamba aliwasilisha ushahidi huo kwa kufuata agizo alilopewa na Spika Justin Muturi mnamo Jumanne alipodai kuwa Naibu Rais hakuwa na hatia ya kunyakua ardhi.

Gedi alikuwa amedai kuwa Ruto alipatikana na hatia ya kunyakua shamba la ekari 100 la Adrian Muteshi mmoja.

"Mkoba huu una ushahidi ambao nitawasilisha kuwa William Ruto alinyakua ardhi hiyo ili Wakenya wajue kuwa hawako salama mikononi mwake," alisema.

Siku ya Jumanne, Gedi alikariri kwamba ana ushahidi wa kuunganisha DP na madai ya unyakuzi wa ardhi.

 

 

 

 

 

View Comments