logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sababu kwa nini 'Covid-19 Billionaires' hawakuwahi kukamatwa- Ruto

Ruto alisema suala la uadilifu lina umuhimu mkubwa kwa muungano wa Kenya Kwanza.

image
na

Yanayojiri02 June 2022 - 11:51

Muhtasari


•Ruto amedai kuwa watu wanaotuhumiwa kuiba pesa zilizokusudiwa kusaidia katika vita dhidi ya Covid-19 hawakukamatwa kwa sababu walikuwa marafiki na ‘watu wanaopigana na ufisadi.’

• Viongozi wakuu wa kisiasa, wakiwemo wanasiasa mashuhuri wa Jubilee, walikuwa miongoni mwa waliofaidika na pesa taslimu za Covid-19. 

DP William Ruto alipofanya mkutano na mabalozi siku ya Alhamisi.

Naibu Rais William Ruto amedai kuwa watu wanaotuhumiwa kuiba pesa zilizokusudiwa kusaidia katika vita dhidi ya Covid-19 hawakuwahi kukamatwa kwa sababu walikuwa marafiki na ‘watu wanaopigana na ufisadi.’ 

Akizungumza alipokutana na mabalozi siku ya Alhamisi, Ruto alisema kuwa urafiki kati yao na watu hao ulifanya iwe vigumu kwa kesi kusonga mbele.

 "Covid bilionares waliponea kwa sababu walikuwa marafiki wa watu ambao walisema wanataka kupigana na ufisadi. Ikiwa vita dhidi ya ufisadi ingeachiwa taasisi, mabilionea wa Covid wanaweza kuwa wamefungwa hivi sasa, "alisema.

Viongozi wakuu wa kisiasa, wakiwemo wanasiasa mashuhuri wa Jubilee, walikuwa miongoni mwa waliofaidika na pesa taslimu za Covid-19. 

Kemsa pia iliangaziwa baada ya kuibuka kuwa maafisa walipeana zabuni kwa mashirika yasiyojulikana chini ya kifuniko cha janga la Covid-19. 

Ruto alisema suala la uadilifu lina umuhimu mkubwa kwa muungano wa Kenya Kwanza.

 "Lazima tushinde vita dhidi ya ufisadi na ndiyo njia pekee ya siku zijazo. Ninakubaliana na rais Uhuru Kenyatta jana kwamba ufisadi unaweza kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo,” akasema. 

“Tunaamini kuwa vita dhidi ya ufisadi lazima ziwe za kitaasisi na sio za kibinafsi. Ni lazima vita dhidi ya wahalifu kutoka pande zote, haipaswi kuwa na silaha dhidi ya mpinzani wako wa kisiasa na watu usiowapenda huku ukiwalinda mafisadi ambao ni washirika wetu au marafiki au watu wa familia yako." 

Ruto ambaye alikuwa akipigia debe Kenya Kwanza alisema iwapo watachaguliwa Agosti 9, watahakikisha kwamba vipengele hivyo vimeondolewa. 

"Tuko wazi katika akili zetu kwamba kuanzisha vita dhidi ya ufisadi ni kufufua uwezo wa mifumo ya uhalifu," alisema.

"Tunahitaji Mahakama isiyolindwa kifedha na ndiyo sababu tutafanya kazi ya hazina ya mahakama ambayo itatoa rasilimali kwa Mahakama kupata programu, vifaa na rasilimali watu." 

DP alisema kwa sasa kuna pengo kubwa la majaji na mahakimu. 

"Kushindwa kupambana na rushwa ni pale unapodhoofisha taasisi za uhalifu kwa kuwa vita dhidi ya washindani wako wa kisiasa," alisema.

(Utafsiri: Samuel Maina)


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved