In Summary

• Monica Wamaitha Gitau, anayesemekana kuwa mmoja kati ya wawaniaji wa uwakilishi wa kike Nairobi alitiwa nguvuni alipoonekana runingani na sare za polisi.

Polisi katika mtaa wa Kilimani jijini Nairobi wamemtia nguvuni mgombea wa uwakilishi wa kike kaunti ya Nairobi aliyetambulika kama Monica Wamaitha Gitau.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, tume ya huduma kwa polisi NPS iliripoti kwamba polisi walidokezewa kuwa Gitau alikuwa anafanya mahojiano ya moja kwa moja kwenye runinga moja humu nchini huku akiwa amevalia vazi rasmi la polisi wa kulinda usalama.

Kulingana na picha zilizopigwa akiwa runingani, polisi walishikwa na kiwewe na hivyo kuwalazimu kumvizia katika kituo hicho ambapo walimtia nguvuni kwa kosa la kuvalia sare za polisi hali ya kuwa yeye si polisi na wala hana kibali cha kuvalia hivyo.

“Maafisa wa polisi walio katika Kituo cha Polisi cha Kilimani leo wamepokea taarifa za mahojiano yanayoendelea katika kituo cha Inooro TV yakimshirikisha mtu anayejifanya kuwa afisa wa polisi wa kike aliyevalia sare kama polisi kupelekea kutilia shaka uaminifu wa mhojiwa hayo,” taarifa ya NPS kupitia Twitter ilisoma.

Mwanasiasa huyo alishikiliwa katika kituo cha polisi cha Kilimali ili kusaidia polisi katika uchunguzi kubaini alikotoa sare hizo za polisi.

Tume ya huduma kwa polisi imevitaka vituo vyote vyahabari kuwa makini na watu wanaowaalika katika stesheni zao kwa ajili ya mahojiano.

Mtu mmoja alisema hii Kenya watu hawaogopi lolote hata bei ya vyakula ikipanda bado wapo tu, kitakachowashtua zaidi Wakenya ni kukatiwa huduma za mtandaoni!

View Comments