In Summary

•Mkuu wa Serikali aliwasili katika Kaunti ya Kakamega mnamo Jumanne, Agosti 2, ambapo atatoa hati hiyo kwa baadhi ya vyuo vikuu katika eneo hilo.

Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta atatoa Hati kwa vyuo vikuu vinane, nusu vikiwa vya umma na vingine vya kibinafsi.

Mkuu wa Serikali aliwasili katika Kaunti ya Kakamega mnamo Jumanne, Agosti 2, ambapo atatoa hati hiyo kwa baadhi ya vyuo vikuu katika eneo hilo.

Vyuo vikuu vinne vya umma ambavyo vitapokea hati ni pamoja na;

1. Kaimosi Friends University (Vihiga County)

2. Alupe University (Busia County),

3. Tom Mboya University (Homa Bay County)

4. Tharaka University (Tharaka Nithi County) 

Vyuo vikuu vinne vya kibinafsi ambavyo vitapokea hati ni pamoja na;

1. Lukenya University (Makueni County)

2. Zetech University (Kiambu County)

3. Kiriri Women's University of Science & Technology (Nairobi County)

4. East African University (Kajiado County).

Rais Kenyatta, ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku 3 Nyanza na Magharibi mwa Kenya.

Atazuru Kampuni ya Sukari ya Nzoia katika Kaunti ya Bungoma kutathmini maendeleo ya ukarabati unaoendelea wa kiwanda cha kusaga sukari kinachomilikiwa na serikali na kukutana na wakulima wa miwa.

Rais pia alipata nafasi ya  kukagua kazi za ukarabati wa njia ya reli kwenye njia ya reli ya Nakuru-Kisumu inayoshughulikiwa na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), na kuhutubia wananchi waliojitokeza kumpokea.

Kisha akaendelea kufungua rasmi Stesheni mpya ya kisasa zaidi ya reli ya Kisumu iliyoko kwenye Barabara ya Busia karibu na Kisumu Cotton Mills (KICOMI).

 

View Comments